Back to top

Waziri Simbachawene agoma kuzindua machinjio ya Msalato Dodoma.

22 January 2020
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.George Simbachawene amesitisha kuzindua machinjio ya Msalato mkoani Dodoma baada ya  kutorishwa na hali ya usafi wa mazingira na majengo yake kujengwa chini ya kiwango.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kamati ya kudumu ya bunge ya viwanda biashara na mazingira kufunga machinjio hayo mapema mwaka jana kutokana na kutokuwa salama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachinjaji na wafanyabiashara katika machinjio hayo wamesema licha ya machinjio hayo kufanyiwa ukarabati bado hali yake si ya kuridhisha huku wakidai wameathirika kiuchumi kutokana na kushindwa kufanya biashara kipindi cha mnada.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Msalato ambapo ndipo machinjio hayo yalipo Bw.Ally Mohamed amesema kuwa wamejipanga ndani ya muda wa wiki kuhakikisha wanakamilisha kwa kiwango chenye ubora machinjio hayo ili yaweze kutumika na wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku.