
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Bw. Donald Wright katika kikao kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya hususani eneo la afya kinga huku Bw.Wright akiahidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 5 kwa Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango mpya wa Global Vaccines wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa chanjo ya Uviko-19.
