Back to top

Waziri Ummy awataka viongozi kutoisubiri serikali

19 July 2018
Share

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka viongozi, kuanzia wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi wao kutambua kwa haraka changamoto zinazowakabili ili kuanza mara moja kuzitatua kuliko kuisubiri serikali

Mhe. Waziri wa afya ametoa kauli hiyo wakati akikagua jengo la akinamama wajawazito wakati wa kujifungua, ambalo limejengwa kwa vyanzo vya ndani litakalokuwa na uwezo wa kulaza akinamama zaidi ya miamoja kwa wakati mmoja ambapo amesema, serikali ni lazima iongeze nguvu.
 
Aidha katika wakati mwingine Mhe. Ummy Mwalimu amesema, serikali ipo pamoja na wadau wanojitokeza kutoa michango kwa ajili ya kuondoa changamoto mbali mbali katika jamii, hivyo, ni wajibu wa kila mwenye fursa kujitokeza kuchangia huduma za kijamii. 

Mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Bw. Abeli Yegi Busalama amesema kuwa, kauli mbiu ya kitabu kilichotungwa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP, I CAN, I MUST, I WILL, ni mwongozo ambao unaiwezesha wilaya ya Kaliua kujiongeza katika kujenga hospitali ya wilaya ili kuwaondolea wananchi changamoto.