Back to top

WAZIRI UMMY: MARUFUKU KUUZA VITABU VYA KLINIKI

10 May 2024
Share

Watendaji wa Wizara ya Afya pamoja na wadau wake wamepigwa marufuku kuwauzia wajawazito vitabu vya kliniki huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitakiwa kuhakikisha vitabu hivyo vinapatikana muda wote.
.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa kadi za maendeleo ya Kliniki kwa wajawazito na watoto, iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

.
“Nimarufuku kuuza vitabu hivi kama ilivyo andikwa kwenye kitabu hiki, Rais Samia ametupatia fedha kwa ajili yakuchapisha vitabu hivi hivyo asipatikane mtu atayepata uchu wa kuuza tena.” Amekemea vikali Mhe. Ummy
.
Amesema suala la mama na mtoto ni kipaumbele cha Serikali kwa sasa ili kuweza kufikia malengo ya milenia, hivyo ugawaji wa kadi za mama mjamzito, watoto wa kike na wakiume ni moja ya hatua zakufikia malengo hayo.
.
Aidha, Waziri Ummy amesema suala la mama na mtoto ni kipaumbele cha Serikali kwa sasa ili kuweza kufikia malengo ya milenia, hivyo ugawaji wa kadi za mama mjamzito, watoto wa kike na wakiume ni moja ya hatua zakufikia malengo hayo.
.
Kuhusu vitabu vilivyo tengenezwa, Waziri Ummy amesema wamezingatia mahitaji yaliopo ambapo inakadiriwa kwa mwaka kuwa na wajawazito Milioni 2 na watoto wanao zaliwa ni Milioni 2.
.
“Kwa sasa mbali yakuboresha Kadi zetu na kuzitofautisha baina ya ile ya mama mjamzito, mtoto wa kiume itakayo kuwa na rangi ya Bluu na ya mtoto wa kike itakayokuwa na rangi ya Pinki.” Amesema Waziri Ummy
.
Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amewataka wa-mama wajawazito kuwahi Kliniki mapema katika miezi Mitatu ya Kwanza ili kuweza kumsadia Mama kujua maendeleo ya ukuaji wa mtoto awapo tumboni.
.
Awali akimkaribisha Waziri Kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, alisema kama kuna kero ilikuwa ikimkwaza Waziri ni pamoja na kukosekana kwa kadi za kliniki hivyo uchapishaji huo ni sehemu yakwenda kuondoa kero hiyo.
.
“Wakinamama wamekuwa wakiacha kwenda Kliniki kwakuwa walikuwa wanauziwa kadi hizi, sasa Serikali imechapisha kadi zakutosha na tutaendelea kufanya hivyo kila mwaka ili kumuepusha Mama na kadhia hii.” Amesema Dkt. Magembe