Back to top

Waziri wa Afya aitaka Bodi mpya ya wadhamini kuiendesha MSD kibiashara

03 December 2018
Share

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.ummy Mwalimu ameitaka bodi mpya ya wadhamini wa bohari ya dawa kuhakikisha MSD inajiendesha kibiashara na kuongeza ufanisi kiutendaji kwa kufuata kanuni na sheria za manunuzi badala ya kila mwaka kutegemea fungu la fedha kutoka serikali 

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipokuwa akizindua bodi hiyo mpya ya wadhamini wa bohari ya dawa ( MSD ) huku akisisitiza suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vya viwango vya kimataifa kwa gharama nafuu zaidi kuliko taasisi nyingine zinazojihusisha na uuzaji na usambazi wa madawa.

Bodi hiyo mpya ya wadhamini wa bohari ya dawa inaongozwa na Dkt.Fatma Mrisho.