Back to top

Waziri wa afya awaonya waganga ukosefu wa dawa Hospitali

22 July 2018
Share

Waziri wa afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa onyo na kuwaagiza waganga wakuu wa wilaya na mikoa kufanya makisio sahihi na kwa wakati ya mahitaji yao ya dawa katika vituo vya afya na hospitali  ili kuepusha malalamiko ya wananchi yanayotokana na uzembe wa baadhi yao unaosababisha kukosekana kwa baadhi ya dawa wakati dawa hizo zinapatikana katika bohari kuu ya dawa MSD. 

Mhe.Ummy Mwalimu ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea vituo vya afya Uvinza na Ilagala pamoja na Zahanati ya kijiji cha Kalenge ambako wadau wa maendeleo shirika la thamini uhai na Engender heath wamesaidia kuboresha miundombinu, utoaji wa huduma na vifaa tiba ambapo amesema serikali imeongeza mgao wa fedha za dawa katika wilaya ya Uvinza kutoka milioni mia moja hadi zaidi ya milioni mia tano ili wananchi watibiwe na sio kuhangaika kukosa dawa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la thamini uhai Dkt. Nguke Mwakatundu amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali kuboresha huduma za afya huku mganga mfawidhi katika zahanati ya kijiji cha Kalenge Judith Kikoti akieleza kuwa kumekuwa na ongezeko la akina mama kujifungulia zahanati kutokana na elimu na hamasa inayotolewa na wadau mbalimbali.