Back to top

Waziri wa maji Mhe.Aweso akiri kupokea miradi mibovu 177.

29 April 2021
Share

Waziri wa maji Mhe.Juma Aweso  amekiri kupokea miradi mibovu 177  katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo ilikuwa inachafua Wizara hiyo na kusababisha adha kubwa ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge katika mkutano wa tatu, kikao cha kumi na tisa cha Bunge, Mhe.Juma Aweso amesema miradi hiyo mibovu ya maji wao waliita kama miradi kichefuchefu.

Miongoni wa wabunge walioibua changamoto hiyo ya maji ni pamoja na mbunge wa jimbo la Namtumbo Mhe.Vita Kawawa aliyetaka kujua lini serikali itamaliza changamoto ya maji katika jimbo la Namtumbo.