Back to top

WCF YAZINDUA MFUMO MATIBABU KIDIJITALI

07 July 2024
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, amezindua mfumo utakaowawezesha wafanyakazi wanaopata madhila wawapo kazini kuweza kupata huduma za matibabu ndani ya saa 24 kupitia mtandao (Medical Service Portal).

Mhe. Ndejembi ambaye alikuwa amefuatana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Zuhra Yunus, amezindua mfumo huo ambao ni sehemu ya maboresho ya utoaji huduma katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwenye banda la Mfuko huo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dae Es Salaam, kwenye viwanja vya Julius Nyerere, maarufu viwanja vya Sabasaba