Back to top

Wenyeviti Kigoma ujiji waomba kushirikishwa katika ukusanyaji mapato.

30 November 2019
Share

Baadhi ya Wenyeviti wa serikali za mtaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiomba serikali kuwashirikisha katika ukusanyaji wa mapato ili kuisaidia Manispaa hiyo kuondokana na tatizo la kushindwa kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wakati pamoja na kupata hati chafu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Wakizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kuongoza kwa awamu ijayo ya miaka mitano katika mitaa yao, wamesema ipo haja ya kuwepo kwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi, tofauti na ilivyokuwa katika kipindi kilichopita ili kuondoa matatizo yanayo wakabili wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la kuapishwa kwa wenyeviti pamoja na wajumbe wa serikali za mtaa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Kigoma, Bwana Jumanne Kitundu amesema chama hicho kimepanga kuwachukulia hatua kali viongozi wa mitaa watakaoshindwa kutekeleza maagizo ya chama hicho na serikali kwa maendeleo ya wananchi.