Back to top

WEZI WA DAWA KUKIONA - DKT. MOLLEL

23 May 2023
Share

Serikali imesema imepanga kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kuhusika na upotevu wa dawa ili iwe funzo kwa wengine wenye nia ovu ambayo huwasababishia wananchi kukosa haki ya msingi ya kupata dawa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel, Bungeni Jijini Dodoma, ambapo amebainisha kuwa, wameendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa bidhaa za Afya, ikiwemo kufunga mifumo ya kielektroniki pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa bidhaa hizo.
.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI, wameendelea kuimarisha kamati za usimamizi wa vituo kwa kuzijengea uwezo, kuhusu majukumu yao katika usimamizi wa bidhaa za Afya.