Back to top

WFP kusitisha msaada wa chakula kwa wakimbizi Sudan Kusini.  

14 September 2021
Share

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema litasitisha kwa miezi mitatu mgao wa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani laki moja nchini Sudan Kusini kuanzia mwezi ujao wa Oktoba kutokana na ukata.
.
Hata hivyo taarifa ya shirika hilo iliyotolewa katika mji mkuu wan chi hiyo Juba, imesema akina mama na watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka miwili wanaoishi kambini wataendelea kupata mgao wa vyakula vyenye virutubisho vya lishe kwa lengo la kukinga na kutibu utapiamlo.

Imesema wakimbizi wa ndani watakaothirika na kitendo hicho ni wale walioko kwenye kambi za Wau, Juba na Bor Kusini na kwamba sitisho hilo litaendelea hadi mwishoni mwa mwaka.