Back to top

WIZARA, SUA ZATEKELEZA MAAGIZO YA MHE. RAIS, DKT. SAMIA

24 May 2023
Share

Kufuatia maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ishirikiane na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kuwawezesha vijana kujiajiri yaanza kutekelezwa baada ya pande hizo mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano kuinua sekta za mifugo na Uvuvi.

Akiongea muda mfupi baada ya kushuhudia tukio la kusaini makubaliano lililofanyika mkoani Morogoro katika Siku ya Kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine Mei 23, 2023 , Waziri wa Mifugo na Uvuvi alisema tukio hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt Samia aliyotoa katika kilele cha Maadhimisho ya NaneNane yaliyofanyika Mkoani Mbeya Agosti 8, 2022. 

Amesema kuwa Dkt.Samia anataka kuona mabadiliko katika sekta za uzalishaji, hivyo fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji zikitumika vizuri  manufaa makubwa yatapatikana ikiwemo kulia kwa  uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Aidha, Waziri Ulega amemshukuru, Mhe. Rais, Dkt. Samia kwa jitihada zake za kuhamasisha vijana na wanawake kushiriki kwenye kilimo kupitia progamu mbalimbali. 

Amesema kuwa Mifugo na Uvuvi ni utajiri kwa sababu matokeo yake ni ya haraka na biashara yake ni ya haraka pia.

Pia, ametoa wito kwa sekta binafsi na washirika wa maendeleo kuendelea kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo ili vijana waweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji kupitia nyanja za kilimo, mifugo na uvuvi.