Back to top

Wizara ya Elimu yatenga Bil.3 'Samia Scholarship'

25 September 2022
Share

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amesema wametenga Bil. 3 zitakazotumika katika mpango wa kufadhili wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani yao ya kidato cha sita kwenye masomo ya sayansi.
.
Waziri Mkenda amesema hayo leo Septemba 25, 2022 ambapo amebainisha kwamba Mpango huo uliopewa jina la 'Samia Scholarship' tangazo lake litafunguliwa rasmi Septemba 27, 2022 na kwa kuanzia watadahili wanafunzi 640.