Back to top

Wizara ya Kilimo yaagizwa kutoa tamko matumizi kamba za Plastiki.

13 September 2021
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kutoa tamko la kisera la zuio la uwepo wa matumizi ya kamba za Plastiki hapa nchini katika kufungashia mazao mbalimbali badala yake zitumike kamba zinazotokana na mkonge.
.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe alipokuwa akizungumza katika mkutano wa pili wa wadau wa sekta ya ya mkonge mwaka huu akimwakilisha Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.
.
Naibu Waziri Bashe ameziagiza wizara, Bodi ya Mkonge pamoja na kituo cha utafiti wa kilimo nchini Mlingano na Halmashauri zote za wilaya zinazolima Mkonge kuhakikisha wanafanya kazi kama timu ili kuleta mapinduzi ya  katika zao la mkonge nchini.
.
Wakieleza matatizo mbalimbali wanazokumbana nayo katika zao la mkonge mwenyekiti wa wadau wa zao hilo, Bw.Damian Luhinda pamoja na mambo mengine ameeleza kuwepo kwa tatizo la tembo kuvamia mkonge kwa fujo.