Back to top

WIZARA YAKAGUA UJENZI JENGO LA WIZARA MTUMBA

17 May 2022
Share

Timu ya Menejiment ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Wizara unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.

Ujenzi wa jengo hilo la ghorofa sita ulioanza Desemba 2021 unatarajia kuchukua muda wa miezi 18 na unafanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Ujumbe wa Menejimenti ya Wizara Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukioongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara Amosy Zephania Mei 17, 2022 ulitembelea maeneo ya ujenzi wa jengo hilo na kupata maelezo kuhusiana na ujenzi huo.

Mhandisi wa ujenzi wa jengo hilo Grace Musita amesema, ujenzi wa jengo hilo la Wizara ya Ardhi ameeleza kuwa umegawanyika sehemu tatu unaendelea vizuri na mwishoni mwa mwezi Mei 2022 wanatarajia kumwaga silabu kwenye sehemu ya kwanza.

"Ujenzi wa jengo unaendelea vizuri na changamoto kubwa ilikuwa ujenzi wa  sehemu ya chini ambayo tumeshaimaliza na mwishoni mwa mwezi huu wa tano tunatarajia kumwaga silabu kwenye sehemu ya kwanza ya jengo"Amesema Grace.

Uzinduzi wa ujenzi wa Ofisi za ghorofa za Wizara eneo la Mtumba awamu ya pili ulifanywa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa wiki ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru.

"Tunataka mji huu wa Serikali uwe rafiki, unaovutia na mabao tunaweza kuusemea popote na ndiyo maana ujenzi wa miundo mbinu yote muhimu unaendelea kwa kasi ukiwemo wa barabara, maji pamoja na umeme"Mhe.Majaliwa amefafanua wakati wa uzinduzi awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan aliidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 300 kwa ajili ya kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu na majengo ya ghorofa yatakayotumiwa na wizara mbailmbali katika mji wa serikali Mtumba.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Mji wa Serikali ikikamilika Aprili 2019 na kuwezesha Wizara na Taasisi mbalimbali kuhamisha ofisi zake mkoani Dodoma.