Back to top

Wizara zishirikiane kupambana na Utapiamlo

10 May 2022
Share

Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Lishe USAID Bi. Debora Niyeha amezitaka Wizara na Taasisi zinazohusiana na masuala ya lishe nchini kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Utapiamlo kuhakikisha jamii na Taifa linakuwa salama.
.
Bi.Debora ameyasema hayo wakati akizungumza katika mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu Mpango wa Pili  Jumuishi wa Masuala ya Lishe wa Kitaifa kwa menejimenti ya sekta ya mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Ukumbi wa Wizara hiyo uliopo Jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa Mpango huo unaanza utekelezaji wake mwaka 2021-2022/ 2025-2026 hivyo kama sekta ya mifugo ina sehemu ya kufanya kuhakikisha malengo ya mpango huo yanafikiwa.
.
Aidha, Bi. Debora aliongeza kwamba vipaumbele katika mpango huo ni Utapiamlo wa chini na wa kuzidi, utapiamlo utokanao na virutubishi na madini kwa kuzingatia makundi yote ndani ya jamii akisema kuwa afya bora huanzia ngani ya familia hadi Taifa huku akisema kwamba bado ipo changamoto kubwa ya lishe hasa kwa watoto chini ya miaka mitano.
.
“Kwa takwimu za mwaka 2018 zinasema asilimia ya watoto 32 ya watoto wa Tanzania wana udumavu, ukondefu watoto zaidi ya 500,000 nchini wanakabiliwa na ukondefu wakati asilimia 45 ya kina mama walio umri wa kuzaa wanakabiliwa na ukosefu wa damu na asilimia 28 ya kina mama wanakabiliwa na uzito uliokithiri ndiyo maana tumekaa kuona namna gani sekta za lishe zinaaweza kutusaidia,”Alisema Mratibu huyo.