Back to top

WIZI WA KUTUMIA SILAHA, YAHYA JELA MIAKA 30

10 July 2024
Share

Yahya Mohamed Matabora (38), mkazi wa Majengo, mkoani Singida, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Mhe.Fadhili Luvinga, ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Singida ,baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo Aprili 24, 2024 ,katika Mtaa wa Jitulize, Kata ya Majengo ,mkoani humo, kwa kunyang'anya mali ya mtu ,huku akitumia silaha, ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi kisha kufikishwa Mahakamani.

Mhe.Luvinga amesema adhabu hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa jamii.