
Timu ya Yanga SC imedaiwa kuwa tayari imeinasa saini ya Nahodha wa Timu ya AS Maniema ya DR-Congo, Maxi Mpia Ngenzeli, ambapo kulingana na mwanahabari mashuhuri nchini humo, Bw.Cedrick Mbala kupitia tovuti ya irisfootball.com, ambaye alifanya mazungumzo na idara ya mawasiliano ya timu ya Maniema, amesema kuwa Ngenzeli ambaye ni mchezaji bora wa Ligi ya Congo 2020/21, tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Yanga.
.
Max Mpia Ngezeli anatajwa kuwa ndiye mrithi wa Bernad Morrison.
.
Wakati huo huo mchezaji Philipe Kinzumbi wa TP Mazembe ambaye nae alikuwa akitajwa kuwaniwa na Yanga ameumalia uvumi huo baada ya jana kuwa ya mmoja ya wachezaji 15 wa TP Mazembe walioanza mazoezi huku akionekana kuwa na furaha.
