
Uongozi wa Klabu ya Yanga, umetoa taarifa za kuachana na Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Hassan Bumbuli kwa utumishi wake ndani ya Klabu hiyo katika kipindi cha miaka 3.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa mkataba wa Bumbuli umekwisha.

