
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesm Mramba amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha zahanati zote nchini zinakuwa na Nishati ya umeme.
Katibu mkuu huyo ameiambia ITV kuwa mpango wa Wizara hiyo ni kupeleka Nishati itakayoweza kufikika kiurahisi katika maeneo hayo ikiwemo ile ya jua ama nyingine yeyote.
Mhandisi Mramba amesema pia Serikali imejipanga kikamilifu kupeleka umeme katika visiwa vyote nchini ili kuwafanya Watanzania waweze kunufaika na nishati hiyo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Nishati kwa sasa Tanzania inatekeleza miradi kadhaa ya nishati ukiwemo wa bwawa la Mwalimu Nyerere na wa Rusumo mkoani Kagera anao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
