Back to top

Zaidi ya Ekari laki moja za zao la Korosho kupandwa wilayani Handeni.

14 April 2018
Share

Zaidi ya ekari laki moja zinatarajiwa kupandwa  zao la Korosho wilayani Handeni kwa msimu huu wa kilimo  ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha zao hilo linakuwa kati ya mazao ya biashara wilayani humo.

Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Handeni wakati wa kukabidhi miche ya mikorosho zaidi ya laki mbili kwa baadhi ya wakulima wilayani hapa ambayo imesafirishwa na magari ya jeshi kutoka mkoani Lindi.

Akipokea miche hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa na hatimae kuigawa kwa wakulima hao mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Godwin Gondwe amesema kuwa wakulima wanatakiwa kuitunza miche hiyo kwani azma ya serikari ni kuhakikisha inawaondolea umaskini wananchi wake.