Back to top

ZAIDI YA MIL.20 KUMTIBU MTOTO MWENYE TATIZO LA MOYO

09 July 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kutoa gari kwa ajili kumfikisha mkoani Dar es Salaam mtoto ambaye ana tatizo la moyo, ambalo gharama zake ni zaidi ya Tsh. Mil.20/=, ili apatiwe matibabu kwa gharama za serikali.
.
Mhe.Mollel ameyasema hayo akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa, ambapo alibainisha kuwa serikali imetatua matatizo mengi ya Afya ambayo yalikuwa lazima uende India au Marekani kutibiwa lakini kwa sasa nchi yetu imekuwa kimbilio kwa mataifa yanayotuzunguka.