Back to top

Zaidi ya Watanzania 345,000 wamechanjwa chanjo ya Corona.

12 September 2021
Share

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema zaidi ya Watanzania 345,000 wamechanja chanjo ya Corona, hivyo serikali inajiandaa kuhakikisha kunakuwa na wiki ya kuchanja lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wengi wanapata chanjo hiyo.
.
Msigwa amesema zoezi la chanjo linaendelea kutolewa lakini kwa sasa kampeni kubwa inafanyika ili kupeleka chanjo vijijini ili kila Mtanzania apate.
.
Katika hatua nyingine Msigwa ameeleza kuwa serikali inakamilisha ujenzi wa Msongo wa Kilovoti 132 wenye urefu wa km 395 kutoka Tabora hadi Kigoma  kupitia Nguruka, mradi huu  utagharimu fedha za ndani kiasi cha TSH Bilioni 69 na utakamilika mwezi Oktoba 2022.
.
Na kuhusu Soko la Kariakoo amesema litakaporudi litakuwa na hadhi ya soko la Kimataifa lenye mazingira mazuri, salama na yanayovutia ambapo wafanyabiashara wataweza kufanya shughuli zao masaa mengi zaidi kama ilivyo kwenye mataifa mengine yaliyoendea.