
Zaidi ya watu milioni 10 tayari wamejisajili kwenye mtandao mpya wa Threads, uliozinduliwa na Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya Instagram, Facebook na WhatsApp, ikiwa na lengo la kuleta upinzani kwa Twitter.
.
Mtandao huo ambao una sifa na unafanya kazi kama Twitter tayari umeanza kutumiwa na watu mashuhuri kama vile Jennifer Lopez, Shakira na Hugh Jackman, pamoja na vyombo vya habari vikiwemo The Washington Post, The Economist na ITV Tanzani (@itvtz).
.
Mtandao huo umezinduliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Meta, Mark Zuckerberg, leo Alhamis, ambapo alitumia saa chache za kwanza za uzinduzi wa mtandao huo, kujibu maswali ya watumiaji wapya.
