Back to top

ZAIDI YA WATUMISHI 700 WA VYETI FEKI WALIPWA

02 December 2022
Share

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umesema tayari umelipa mafao kwa zaidi ya watumishi 700 waliofutiwa ajira kwa kukosa vyeti halali, baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuelekeza watumishi hao kupatiwa mafao ya michango yao waliyochangia katika kipindi chao cha ajira.

Hayo yamebainishwa Jijini Arusha na Meneja Mahusiano wa PSSSF, James Mlowe, na kusema fedha hizo zinazoendelea kulipwa ni kati ya zaidi ya bilioni 22 zinazopaswa kulipwa wa watumishi 9,700, ambao taarifa zao zimeshafanyiwa uhakiki.

Mlowe amewatahadharisha wastaafu wanaosubiri mafao yao kujieupusha na matapeli wa mtandanaoni, wanaowalaghai na kuchukua fedha kwa ahadi za kuharakishiwa mchakato wa kulipwa mafao.

Ameongeza kuwa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma PSSSF ni zao la mifuko mitatu iliyokuwa ikitoa huduma kwa watumishi wa umma ambayo, iliunganishwa mnamo mwaka 2018 kwa lengo la kuwa na uwiano wa mafao kwa watumishi na kwa sasa unalipa kiasi cha bilioni 60 za pensheni kila mwezi kwa wastaafu 158.