
Wanaikolojia wamegundua zana za mawe zilizotumika miaka milioni mbili iliyopita na binadamu wa kale zaidi katika eneo la Bonde la Olduvai, Kaskazini mwa Tanzania.
.
Ugunduzi huo unatoa mwanga mpya juu ya namna binadamu wanaoaminika kuwa ni wa kale zaidi walivyoishi na kuyamudu mazingira yao. Ugunduzi huo pia unatoa jibu la kwamba, binadamu wa kale aliishi miaka milioni mbili iliyopita na sio milioni 1.8 kama ilivyogundulika na watafiti wa awali.
.
Ugunduzi huo ni matokeo ya utafiti uliochukua miaka mitatu na ulihusisha watafiti kutoka ndani na nje ya Tanzania.
BBC Swahili