
Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imejiandaa kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kuyapokea mabadiliko ya teknolojia ambayo ni msingi muhimu kwa kukuza na kuendeleza uchumi wa kisasa pamoja na kurahisisha maisha ya wananchi wa hali zote.
.
Mwinyi ameyasema hayo leo Julai 29, 2023, kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Kidijitali wa Serikali na Mfumo wa Bajeti na Matumizi Serikalini (BAMAS) iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Mkoa wa Mjini Magharibi.
.
Aidha, Rais Mwinyi amebainisha kuwa mfumo wa BAMAS umeleta uwazi kwenye matumizi Serikalini, utaimarisha uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali, umewezesha mifumo yote ya malipo na matumizi ya fedha za Serikali kusomana kwa haraka na kwa ufanisi.
