
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amewafuta kazi Mkuu wa Huduma za Ujasusi na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ambapo amebainisha kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kubainika kwamba baadhi ya maafisa kutoka idara za wakuu hao walikuwa wakishirikiana na Russia.
.
Aidha, Zelenskyy amesema kuwa kesi 651 za jinai zimefunguliwa zikiwahusisha wafanyakazi katika ofisi ya mwendesha mashtaka, vitengo vya kuchunguza kesi na taasisi nyingine za kisheria.
