Back to top

ZIARA YA INDIA KUFUNGUA NJIA KISIASA, KIUCHUMI.

09 October 2023
Share

Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, amesema ziara yake ya Kiserikali nchini India, inalenga kufungua njia mpya za maendeleo ya kisiasa na kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Baada ya kutambulishwa rasmi kwa maafisa wakuu wa nchi mwenyeji, Rais ameviambia vyombo vya habari vya India kwamba, nchi hizo mbili zinatabiri ushirikiano wa kimkakati kupitia ushirikiano wao wa kiuchumi.

Rais amesema hayo  nchini India Oktoba 9, 2023, alipokuwa akikaribishwa kwa heshima za kijeshi.

Rais Samia ameongeza kuwa, Tanzania inatarajia uhusiano uliopo wa nchi hizo mbili ulioasisiwa na waasisi, Mwalimu Julius Nyerere na Mahatma Ghadhi utaendelea kwa miongo mingi zaidi

Rais Samia kwa sasa yuko India kwa ziara yake ya kwanza  nchini humo, iliyoanza Jumapili, Oktoba 8, 2023, na itakamilika Oktoba 11, 2023.

Nchi hiyo ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Tanzania na biashara kati ya nchi hizo mbili ambayo sasa inafikia dola bilioni 6.4.