
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema ziara ya Mawaziri wa Kisekta ambayo ni mwendelezo wake katika kutembelea maeneo yenye migogoro itafika katika Msitu wa Kazimzumbwi zamu yake itakapofika kusaidia kutatua changamoto ya mgogoro uliopo baina ya wananchi wa vijiji vilivyo pembezoni mwa Msitu huo na Wakala wa Uhifadhi wa Misitu (TFS).
Naibu Waziri Masanja amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa juu ya Mpango wa serikali katika kutatua mgogoro huo.
