Back to top

ZIARA:Kamati ya maadili ya MCT yatembelea ITV.

27 March 2018
Share

Kamati ya Madili ya Baraza la Habari Tanzania MCT ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Jaji Mstaafu Jukson Mlay imetembelea vyombo vya habari vya IPP na kuelezea kuridhishwa na uwekezaji wa vyombo hivyo pamoja na kufuata misingi ya taaluma ya uandishi wa habari ikiwemo misingi ya maadili katika uandishi na utayarishaji wa habari na vipindi.