
Serikali imewataka wazazi kuzingatia lishe bora kwa watoto, ambapo imewasisitiza kusimamia zoezi hilo kuanzia kwenye utungaji wa mimba ili kumsaidia mtoto, hata baada ya kuzaliwa na wakati yuko shule, ubongo na akili yake kufanya kazi kikamilifu.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, mkoani Dar es Salaam, wakati akipokea vidonge vya matone ya Vitamini A, kutoka kwa shirika la Nutritrion International (NI) kwa ajili ya kuwapatie watoto walio na umri chini ya miaka 5, wapatao milioni 11 kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili na kuimarisha afya ya macho.
.
Aidha Dkt. Mollel, amewataka Watanzania kuzingatia milo yao ya kila siku kwa kupata chakula chenye lishe hasa vyenye vitamini ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kisukari.
.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho kikwete, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Menejimenti nchini ya shirika la Nutrition International (NI), amesema shirika hilo limeipatia Serikali vidonge vya matone vya Vitamini A milioni 22.
