Back to top

Zoezi la kuhamisha mali Twiga Bancorp kukamilika ndani ya miezi 3

17 May 2018
Share

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Bwana Sabasaba Moshingi amesema zoezi la kuhamisha wateja, wali na wafanyakazi wa iliyokuwa benki ya Twiga Bancorp itakamilika ndani ya miezi mitatu.

Amesema waliokuwa wateja wa Benki ya Twiga wapo katika mikono salama huku akiwataka wafanyakazi 100 waliokuwa Benki ya Twiga kuungana na wenzao 800 wa TPB katika kuifanya benki ya TPB PLC kuimarika zaidi.

Bwana. Moshingi ameongeza kuwa katika kipindi hicho kila kitu kitakuwa kimekamilika ikiwemo kuunganisha mifumo ya Kompyuta.

Jana benki kuu ilitangaza kuziunganisha benki ya Twiga iliyokuwa chini ya usimamizi wa benki kuu na Benki ya TPB PLC.