Back to top

Zoezi la uvaaji barakoa shuleni lapuuzwa

29 June 2020
Share

Zoezi la uvaaji barakoa katika shule za msingi na sekondari ikiwemo  kila mwanafunzi kukaa umbali wa mita moja ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona wilayani Lushoto,limeshindwa kufikiwa kutokana na changamoto mbalimbali baada ya shule zote nchini kufunguliwa.

Wakizungumza katika shule tofauti ambazo ITV imetembelea ili kuhakiki maelekezo ya wizara ya afya na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona mashuleni,baadhi ya wadau wamesema uwekeji wa maji tiririka umefanikiwa lakini changamoto ni uhaba wa vyumba vya madarasa.

Katika zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Januari Lugangika amesema siku moja kabla ya shule kufunguliwa amehimiza tahadhari kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na uvaaji barakoa na kukaa umbali wa mita moja.