Back to top

EWURA YAFIKA MASWA KUTATHMINI BEI YA MAJI.

30 January 2024
Share

Timu ya watalam kutoka EWURA imefika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, kufuatilia na kufanya tathmini ya kina juu ya swala la bili za maji, lililolalamikiwa na wananchi wa mji wa Maswa kwamba Mamlaka ya Maji ya Maswa inawatoza bili kubwa ya maji.

Timu hiyo imefika mkoani humo, baada ya Malalamiko hayo kumfikia Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso na kutoa ahadi kwamba ndani ya siku moja Mamlaka inayohusika na upangaji wa Bei ya Maji EWURA ingefika kufanya tathmini upya na kuja na ushauri juu ya kiwango sahihi cha wananchi kuchangia huduma ya Maji.

Januari 29, 2024 wananchi wa mji wa Maswa waliwasilisha malalamiko yao kwa Katibu Mwenezi (CCM) Ndg.Paul Makonda na malalamiko hayo kufikishwa kwa waziri moja kwa moja.