Back to top

RAIS WA NAMIBIA HAGE GEINGOB AFARIKI DUNIA

04 February 2024
Share

Rais wa Namibia, Hage Geingob, amefariki dunia, leo Februari 04, 2024, wakati akipatiwa matibabu ya saratani katika hospitali ya Lady Pohamba, iliyopo Jijini Windhoek nchini humo.
.
Taarifa za kifo cha Geingob zimetangazwa na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Nangolo Mbumba, ambapo amebainisha kuwa Geingob alifariki mapema alfajiri, akiwa karibu na mkewe Monica Geingob pamoja na watoto wake.
.
Rais Geingob, amefariki akiwa na umri wa miaka 82, na kwamba alikuwa akitumikia muhula wake wa pili na wa mwisho kwenye nafasi hiyo, ambayo aliapishwa mnamo 2015.
.
Ikumbukwe Kiongozi huyo aligunduliwa kuugua saratani na alitangaza hali yake mbele ya umma mwezi uliopita na ofisi yake ilitangaza kwamba atasafiri kuelekea Marekani kupata matibabu, na kwamba atarejea Namibia Februari 2, 2024.