
Shirika la Hisani la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), limesema Watoto 13 hupoteza maisha kila siku, kutokana na utapiamlo uliokithiri katika kambi ya Zamzam, huko Darfur Kaskazini mwa Sudan.
Shirika hilo limesema kuwa hayo ni matokeo ya vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 10 nchini humo.
Mkuu wa Kitengo cha dharura cha MSF, nchini Sudan, Claire Nicolet mtoto mmoja hupoteza maisha kila baada ya saa mbili katika kambi hiyo, na kwamba wale wenye utapiamlo uliokithiri na ambao bado wako hai, wako hatarini zaidi kupoteza maisha ndani ya wiki tatu hadi sita ikiwa hawatapatiwa matibabu.
#DW
