Back to top

TEMESA FUNGENI MIFUMO KUDHIBITI WIZI

06 February 2024
Share

Waziri wa Ujenzi, Mhe.Innocent Bashungwa, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha karakana zote za TEMESA zinafungwa mifumo ya teknolojia inayoweza kudhibiti vitendo vya udanganyifu pamoja na wizi wa vipuli unaofanywa na watumishi wa Wakala huyo, wasio waaminifu, hali inayosababisha malalamiko makubwa kwa wateja.
.
Mhe.Bashungwa ametoa maagizo hayo, Jijini Dodoma wakati akizungumza na Menejimenti ya Watumishi wa TEMESA ambapo amewataka Mameneja wa Mikoa wa Wakala huo nchi nzima kuboresha huduma za vivuko na usimamizi wa mitambo kwenye karakana zake.