
Mawaziri sita wa wizara tofauti pamoja na baadhi ya maafisa wa idara za ulinzi na usalama nchini wameanza kikao mkoani Dodoma leo kujadili sakata la Korosho zilizokutwa vietnam zikiwa na kokoto.
Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba, Mawaziri hao wanakutana kujadili sambamba na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kulimaliza suala hilo na kuzuia matukio kama hayo kutokea.
Amesema baada ya kikao hicho maazimio ambayo watakuwa wameyafikia watayawasilisha kwa Waziri Mkuu Mhe.Khasim Majaliwa ili Serikali itoea tamko la pamoja kuhusiana na usafirishaji wa Korosho.
Katika hatua nyingine, Waziri Dkt.Tizeba amesema maonesho ya wakulima yaani nane nane kwa mwaka huu na mwakani yatafanyikia mkoani Simiyu na amewaomba wanaotaka kushiriki maonesho hayo kuanza ujenzi wa mabanda eneo la yatakapofanyikia.