Back to top

CHADEMA KUMUENZI LOWASSA KWA MAANDAMANO

13 February 2024
Share

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema licha ya Taifa kuwa katika msiba wa kifo cha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, bado adhma kufanya maandamano ya amani katika Mkoa wa Mwanza iko palepale na kuahidi kuwa watatumia siku hiyo kumuenzi na kuimarisha demokrasia aliyokuwa akiishi Kiongozi huyo.
.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, pamoja na wanachama na wasiokuwa wanachama wa chama hicho akiwemo Wilbroad Silaa wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo, yatakayofanyika siku ya Alhamisi, Februari 15, 2024.