
Mahakama ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani, imemuhukumu kifungo cha maisha Jela, Winston Mpiluka Willium (32) mkazi wa Mlamleni Mkuranga kwa kosa la kulawiti Mwanafunzi wa miaka (11)
Mahakama hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa alimlawiti mtoto huyo baada ya kumuita nyumbani kwake na kumfungia ndani kisha kumfanyia kitendo hicho cha kinyama na kumwambia asiseme na kumpa shilingi 200 hadi 700 au maziwa ya ng'ombe kwani mtuhumiwa alikuwa mchunga ng'ombe.
Kesi ilisikilizwa na upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano ambao walithibitisha kosa na mtuhumiwa alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria ambapo Mbele ya Mhe.Herieth Mwailolo - SRM, Mahakama imemhukumu kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wengine.
