
Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya, wametakiwa kuhakikisha wanasimamia na kuimarisha mawasiliano baina ya mtoa huduma na mpewa huduma kwa kuzingatia matumizi ya lugha zenye staha.
.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt.John Jingu, kwenye mkutano na wa mwaka wa waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, uliofanyika Jijini Dodoma.
.
Dkt.Jingu amesema kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya watoa huduma ambapo wamekuwa wakitumia lugha ambazo si za staha wakati wakiwahudumia wateja hali amabyo inasababisha kupoteza rasilimali kwa kufanya uchunguzi wa matendo hayo badala ya kuboresha huduma.
.
Aidha Dkt.Jingu amelaani vitendo vya baadhi ya watoa huduma za afya nchini kuendekeza matumizi ya simu hasa wawapo katika maeneo ya kazi
