Back to top

RAIS SAMIA AWASILI ADDIS ABABA, NCHINI ETHIOPIA

18 February 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, amewasili Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika.
.
Rais Samia ameenda nchini Ethiopia mara tu baada ya kutoka Ngarashi mkoani Arusha, ambapo aliongoza waombolezaji katika maziko ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa.
.
Katika mkutano huo, Rais Samia na Viongozi wengine wa Afrika watajadili kuhusu amani na usalama wa nchi za Afrika, pamoja na sera na majawabu kuhusu elimu na ujuzi, maeneo ambayo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wakazi zaidi ya bilioni moja wa nchi wanachama.