Back to top

RAIS MWINYI:SEKTA BINAFSI NI MDAU WA UCHUMI NA MAENDELEO.

19 February 2024
Share

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaiangalia sekta binafsi kwa mtazamo chanya, wa kuwa mdau muhimu wa uchumi na maendeleo.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo, alipofungua Mkutano mkuu wa kumi na tano (15) wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa tayari kazi ya kuandaa sheria inayohusisha maendeleo ya sekta binafsi inaendelea chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ikisimamiwa na Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Biashara.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kuitangaza Zanzibar katika majukwaa mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa kuvutia wawekezaji wengi zaidi ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.