Wafusi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema ambao wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ili kujua hatima ya dhamana ya viongozi waandamizi sita wa CHADEMA ambao wameshtakiwa kwa makosa nane likiwemo la UCHOCHEZI wa UASI wamezuliwa kungia ndani ya viwanja vya Mahakama.
Baada ya kutakiwa kuondoka wafuasi hao wamegoma kuondoka na kubakia nje ya geti kuu la kuingia ndani ya Mahakama na kuanza kuimba nyimbo mbalimabli licha ya polisi kuwataka kuondoka eneo hilo mara moja.