
Utawala wa kijeshi nchini Guinea, hapo jana umetangaza kuivunja Serikali iliyokuwepo tangu Julai 16, 2022 na kwamba inatarajiwa kutangaza safu mpya ya uongozi katika siku chache zijazo.
Taarifa hiyo ilitangazwa kwenye runinga ya kitaifa na Afisa Mkuu wa Utawala wa kijeshi nchini humo, Brigedia Jenerali Amara Camara, tangazo lililowashtua wengi.
Hata hivyo haijabainika nini sababu za kuvunjwa kwa serikali hiyo na aliyekuwa Waziri Mkuu Bernard Goumou aliyechukua nafasi ya Mohamed Béavogui, ambaye alilazimika kuondoka ofisini kwa sababu za kiafya.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, agizo la Rais Mamady Doumbouya, linasema kuanzia Jumatatu ya Februari 19 ni makatibu wa Baraza la Mawaziri na wasaidizi wao wakuu ndio wamepewa jukumu la kushughulikia shughuli zote za serikali.
