
Serikali imempa miezi miwili Mkandarasi anayejenga Barabara ya Mikumi-Kidatu-Ifakara, sehemu ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango cha lami na Daraja la Mto Ruaha Mkuu kukamilisha Ujenzi huo kutokana na mkandarasi huyo kuwa nje ya muda wa mkataba.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Mh. Innocent Bashungwa wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kukagua Barabara hiyo na Daraja la Mto Ruaha Mkuu na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi.






Aidha, Bashungwa ameongeza kuwa Mkandarasi huyo wa Kampuni ya M/s Reynolds Construction Company, ameshalipwa Fedha zote za kutekeleza mradi huo kwa wakati na daraja hilo linajengwa kwa viwango imara Sambamba na ujenzi wa barabara zake.
Akitoa Taarifa ya Mradi, Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Alinanuswe Kyamba, amesema ujenzi wa barabara hii unafadhiliwa na mfuko wa maendeleo wa Nchi za ulaya, ukishirikiana na shirika la Msaada la Uingereza ( UKAID) pamoja na Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa( USAID).
