Back to top

AJALI ARUSHA: RAIS AAGIZA MAJERUHI WATIBIWE BURE

25 February 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kuwa majeruhi wote wa ajali iliyohusisha magari manne katika eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha, wapewe matibabu bila kulipa  gharama zozote.  
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt.Godwin Mollel, alipofika kuwajulia hali majeruhi 21 wa ajali hiyo, waliolazwa katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru, ambapo ameeleza kuwa majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndiye kapewa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC, Mkoani Moshi. 


Akizungumza baada ya kusikiliza maelekezo hayo, mmoja wa majeruhi, Raia wa Togo, aliyejitambulisha kwa jina la  Apelo Apeto (32), ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa huduma bora waliyompatia na anayoendelea kupatiwa hospitalini hapo.
.


"Kwa ajali hii ningekuwa nchini kwetu tayari ningekuwa  nimepoteza  maisha kwani  kule  bila kilipia  huduma za matibabu hupatiwi huduma, lakini  kwa Tanzania walivyowakarimu na weledi wameweza  kuokoa maisha yangu  mpaka sasa naendelea  vizuri na naweza  kuongea", ameeleza Apeto


.
Raia huyo amesema alikuja  nchini  Tanzania  kwa semina  ya mafunzo  ya Uongozi iliyokuwa ikifanyika mkoani  hapo na baadaye  wakaenda  kufanya  utalii  wa kuangalia kabila la wamasai wakati wanarudi ndo wakapata ajali hiyo.