
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini (TRC), Bw.Masanja Kadogosa amesema Watanzania wasiwe na wasiwasi wa kwamba treni inaweza kuzimika ikiwa njiani kisa umeme, kwa sababu njia ya umeme (Transmission Line), unaotumika katika kuendesha Treni ya Umeme ya Kisasa ya (SGR), inajitegemea.
.
Bw.Kadogosa ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa safari ya majaribio ya treni hiyo kutoka mkoani Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro.
.
Amesema ili treni isimame kwa sababu ya umeme labda kama nchi nzima umeme uwe umekatika jambo ambalo sio rahisi kutokea.
