
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Dkt. Abiy Ahmed Ali anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 29 Februari hadi 02 Machi, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi Ikulu, Dar es Salaam tarehe 01 Machi, 2024 na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Lengo la ziara hii mbali na kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, inalenga pia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ethiopia ambazo zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya biashara na uwekezaji, elimu, utamaduni, usafirishaji wa anga, kilimo, mifugo, udhibiti wa uhamiaji holela, ulinzi na usalama.
Aidha, katika sekta ya elimu ziara hii, itaziwezesha nchi hizi mbili kubadilishana wanafunzi na kujenga uwezo, katika uuandaji wa mitaala na Tanzania, kupata fursa ya kufundisha Kiswahili nchini Ethiopia.
